1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Majeshi ya waasi yatishia kuyashambulia majeshi ya AU.

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBee

Umoja wa Afrika umesema jana Ijumaa kuwa umepokea vitisho mbali mbali kutoka kwa makundi ya waasi dhidi ya ujumbe wake wa kulinda amani katika jimbo lililokumbwa na ghasia la Darfur nchini Sudan.

Umoja wa Afrika umesema kundi la Sudan Liberation Army , wanaharakati wanaofanyakazi pamoja na jeshi la kulinda amani , wametishia jeshi hilo baada ya kupunguzwa kwa maslahi ya masurufu ya jeshi hilo la waasi kutokana na upungufu wa fedha.

Katika taarifa umoja wa Afrika umesema kuwa unachukulia kitisho hicho kwa dhati na unapenda kusisitiza kuwa kundi lolote litawajibika na hatua kama hizo zinazofikiriwa sasa ama kuchukuliwa wakati wowote hapo baadaye.

Waasi wamewauwa wanajeshi kadha wa umoja wa Afrika wanaolinda amani katika jimbo la Darfur tangu jeshi hilo kufika katika eneo hilo.