1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Matumaini ya kupeleka Darfur vikosi vya Umoja wa Mataifa

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCs2

Kuna matarajio kuwa mazungumzo yanayohusika na suala la kupeleka vikosi vya Umoja wa Mataifa kuvisaidia vile vya Umoja wa Afrika katika jimbo la mgogoro la Darfur nchini Sudan yanafanikiwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan nchini Ethiopia,aliufungua mkutano huo mjini Addis Ababa kujadili mradi mpya unaopendekeza kuwa na wanajeshi 20,000 wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kulinda amani katika jimbo la Darfur kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa.Zaidi ya watu 200,000 wamepoteza maisha yao katika mgogoro wa miaka mitatu katika jimbo hilo magharibi mwa Sudan. Hivi karibuni,mashambulio yaliofanywa na vikosi vya serikali na makundi ya waasi yameongezeka. Lakini serikali ya Sudan inadai kuwa inawanyanganya silaha wanamgambo wa Kiarabu wanaotuhumiwa kufanya mauaji hayo kwa niaba ya serikali.Mamlaka ya vikosi vya hivi sasa vya Umoja wa Afrika vilivyoshindwa kuzuia mmuagiko wa damu,yanamalizika mwisho wa mwaka huu.