1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADELAIDE: Baba wa mfungwa amekosoa kesi ya Guantanamo

31 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCDh

Baba wa mfungwa David Hicks,aliekutikana na hatia ya ugaidi kwenye Mahakama ya Kijeshi ya Marekani ya Guantanamo,ameikosoa kesi ya mwanae.Terry Hicks amesema adhabu ya kifungo cha miezi tisa aliyopewa David Hicks hudhihirisha udhaifu wa ushahidi wa kesi hiyo.Muastralia David Hicks katika maafikiano ya kukiri makosa,amekubali kufuta madai yake kuwa aliteswa alipokuwa kizuizini na pia hatozungumza na vyombo vya habari kwa muda wa mwaka mmoja na hatoishtaki serikali ya Marekani.Sasa Marekani katika muda wa siku 60 zijazo inapaswa kumpeleka David Hicks nyumbani Australia,ambako atatumikia kifungo kilichopunguzwa kuwa miezi tisa.Hicks ambae ameslimu,alikamatwa nchini Afghanistan Desemba mwaka 2001 na ni mfungwa wa kwanza wa jela ya Guantanamo,kufikishwa mbele ya mahakama iliyoundwa kusikiliza kesi za wafungwa wanaoshukiwa kuhusika na ugaidi.