1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magezeti ya Ujerumani.

Abdu Said Mtullya15 Machi 2013

Wiki hii magazeti ya Ujerumani yameandika juu ya kitendawili cha kidiplomasia kuhusu Rais mteule wa Kenya Kenyatta, na juu ya makubaliano yaliyofikiwa na nchi mbili za Sudan kuhusu ugavi wa mafuta.

https://p.dw.com/p/17yZt
Rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais Mteule wa Kenya Uhuru KenyattaPicha: REUTERS

Gazeti la "Neues Deutchland" linayatilia maanani mambo mawili kuhusu Kenya.

Kwanza hatua ya mgombea alieshindwa, Raila Odinga ya kuyatilia mashaka matokeo ya uchaguzi. Odinga amesema ataenda mahakamani ili kuyapinga matokeo. Jambo la pili ni kwamba Rais mteule Kenyatta anakabiliwa na mashtaka kwenye Mahakama Kuu ya mjini The Hague ICC.

Gazeti la "Neues Deutschland" linasema mashtaka yanayowakabili Rais mtuele Kenyatta na makamu wake William Ruto yanaweza kusababisha athari za kiuchumi kwa Kenya. Gazeti hilo limefahamisha kwamba Umoja wa Ulaya unafikiria kuyaweka mawasialiano yake na Uhuru Kenyatta katika kiwango cha chini kabisa atakapoanza kazi. Lakini gazeti la"Neues Deutchland" limesema katika makala yake kwamba kuchaguliwa kwa Kenyatta ni matokeo ya kura ya maoni dhidi ya Mahakama Kuu ya mjini The Hague ,ICC.

Marekani haitamtenga Kenyatta

Gazeti la "Frankfurter Allgemeine "pia limechapisha makala juu ya kitendawili cha kidiplomasia baina ya Marekani na Kenya chini ya uongozi wa Uhuru Kenyatta. Gazeti hilo linaeleza kuwa Kenya ni mshirika muhimu wa Marekani katika harakati za kupambana na ugaidi barani Afrika.Lakini ushirikiano katika harakati hizo utaendelea vipi wakati Kenyatta anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu kwenye Mahakama Kuu ya kimataifa ya mjini The Hague?

U.S. Secretary of State John Kerry speaks during a joint news conference with Qatar's Prime Minister and Foreign Minister Sheikh Hamad bin Jassim bin al-Thani in Doha March 5, 2013. Kerry said on Tuesday Washington was increasingly confident that weapons being sent by others to the Syrian opposition were going to moderate forces within it rather than to extremists. REUTERS/Stringer (QATAR - Tags: POLITICS)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John KerryPicha: Reuters

Gazeti la "Frankfurter Allgemeine" limemnukuu mshauri wa Marekani juu ya masuala ya Afrika Johnnie Carson akiashiria kwamba utawala wa Marekani hautachukua hatua zozote zinazoweza kuwa na maana ya kumtenga kabisa Rais mteule Uhuru Kenyatta.

Amani na mafuta baina ya nchi mbilzi za Sudan:

Gazeti la "die tageszeitung" limechapisha taarifa juu ya mkataba uliofikiwa baina ya Sudan na Sudan ya Kusini juu ya ugavi wa mafuta.Pamoja na suala la mafuta, Sudan ya Kusini imekubali kuyaondoa majeshi yake kutoka kwenye mpaka.

Gazeti la "die tageszeitung" limearifu kwamba nchi mbili za Sudan zilitiliana saini, mjini Addis Ababa,mkataba juu ya mafuta na kuleta usalama.Kwa mujibu wa mkataba huo,mafuta kutoka Sudan ya kusini yataanza kusafirishwa tena hadi Sudan baada ya shughuli hiyo kusimamishwa kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja.Hata hivyo gazeti la "die tageszeitung" limetilia maanani katika taarifa yake kwamba suala la jimbo la Abyei bado halijapatiwa ufumbuzi.Jee jimbo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta litakuwa katika upande gani?

Mwanamichezo Henry Wanyoike:

Gazeti la"General Anzeiger" wiki hii limechapisha makala juu ya mwanamichezo wa Kenya, Henry Wanyoike.Jee yeye ni nani hasa?

Bildunterschrift: Henry Wanyoike im Interview mit der DW Stichwort: Paralympics, blinder Marathonläufer, Henry Wanyoike, Sportler Kenia, blind marathon runner, Kenya Paralympics Sie wurden von dem Korrespondent der Kisuaheli Redaktion, Alfred Kiti, in Nairobi gemacht. Er überträgt der DW die Rechte an den Fotos .
Mwanamichezo Henry Wanyoike akihojiwa na DWPicha: DW

Gazeti hilo linaeleza kuwa Henry Wanyoike ni mlemavu wa macho anaekimbia mbio ndefu. Ameshafanikiwa kushinda medali za dhahabu mara nne katika mashindano ya walemavu ya Paralimpiki. Gazeti la "General Anzeiger" linaarifu kuwa mwanamichezo huyo amejifunza kuielewa vizuri hali yake na kuigeuza kuwa nguvu ya kumwezesha kupambana na umasikini nchini mwake, Kenya.

Kutokana na mafanikio yake,wasifu wake umetengenezewa filamu inayoonyeshwa kwenye kumbi za sinema nchini Ujerumani.Filamu hiyo inaitwa "Go for Gold"

Wanyoke alipofuka baada ya kukumbwa na kiarusi muda mfupi kabla ya kutimiza umri wa miaka 21. Kutokana hali hiyo alilazimika kuiacha kazi yake ya ufundi wa viatu. Wanyoike hakukata tamaa na aliamua kuingia katika michezo.

Wanyoike aliibuka mshindi wa mbio za mita 5,000 kwenye mashindano ya walemavu mjini Sydney mnamo mwaka wa 2000. Tokea wakati huo ameshinda mara kadhaa. Dhamira yake ni kuwahamasisha na kuwasaidia watu wengine nchini Kenya.Na kwa ajili hiyo ameuzindua wakfu unaoitwa"Henry Wanyoike Foundation." Wakfu huo unalipia upasuaji wa kuepusha ulemavu wa macho nchini Kenya,na hasa miongoni mwa watoto.

Mwandishi: Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen/
Mhariri: Mohammed Khelef