1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rugby: Springboks yamaliza ya tatu katika Kombe la Dunia

31 Oktoba 2015

Afrika Kusini imemaliza katika nafasi ya tatu na kuchukua nishani ya shaba katika Kombe la Dunia la mchezo wa Rugby baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Argentina. New Zealand itachuana na Australia katika fainali

https://p.dw.com/p/1GxZv
Rugby, WM, Spiel um Platz 3: Südafrika - Argentinien 24:13
Picha: Reuters

Afrika Kusini iliizidi nguvu Argentina kwa pointi 24 kwa 13, katika mpambano wa kumtafuta mshindi wa nafasi ya tatu hapo jana katika uwanja wa Olimpiki.

Licha ya ushindi huo, mchezaji wa Springboks Bryan Habana hakuweza kutwaa tena rekodi ya kufunga trai nyingi zaidi katika Kombe la Dunia.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 32 alijaribu juu chini kupata trai lakini hakufua dafu. Afrika Kusini ilitumia kikosi chake bora cha kwanza na ubabe wake ulidhihirika wazi katika mechi hiyo iliyochezewa mashariki mwa London.

Macho sasa yanaelekezwa kwa mechi ya kali ya kukata na shoka ambayo ni fainali kati ya New Zealand na Australia hivi leo uwanjani Twickenham

Mwandishi: Bruce Amani/DPA
Mhariri: Mohamed Dahman