1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika ya kati ; makubaliano yatiwa saini

13 Januari 2013

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize amemfuta kazi waziri wake mkuu na kulivunja baraza lake la mawaziri Jumamosi(12.01.2013)akisafisha njia kwa kuteuliwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

https://p.dw.com/p/17J4a
Central African Republic President Francois Bozize, right, shakes hands with Michel Djotodia, leader of the Seleka rebel alliance, as heads of state and other participants applaud, during peace talks in Libreville, Gabon, Friday, Jan. 11, 2013. Officials say that the rebel group controlling much of the northern half of the country have agreed to enter into a coalition with the government. The deal will allow President Francois Bozize to stay in office until his current term expires in 2016. (Foto:Joel Bouopda Tatou/AP/dapd)
Makubaliano yatiwa saini mjini Libreville GabonPicha: dapd

Serikali  na  waasi  wa  muungano  wa  Seleka , ambao  walisonga mbele  katika  mashambulizi  yao  hadi  karibu  na  mji  mkuu  Bangui mwezi  uliopita, wamekubaliana  kuunda  serikali  ya  mpito mwishoni mwa   mazungumzo  yao  yaliyofanyika  katika  mji  mkuu  wa  Gabon , Libraville  siku  ya  Ijumaa(11.01.2013).

"Kiongozi  wa  nchi, ameondoa matumizi  ya  amri  iliyotolewa  Aprili  22, 2011, inayohusiana  na  kuteuliwa  kwa  serikali," imesema  amri  ya  rais iliyosomwa  katika  televisheni  ya  taifa.

Central African Republic peace talk participants, including Seleka rebel alliance leader Michel Djotodia, left, and Jean Willybiro Sako, second left, head of the Central African Republic's government delegation, sign a peace agreement, in Libreville, Gabon, Friday, Jan. 11, 2013. Officials say that the rebel group controlling much of the northern half of the Central African Republic have agreed to enter into a coalition with the government. The deal will allow President Francois Bozize to stay in office until his current term expires in 2016. (AP Photo/Joel Bouopda Tatou)
Viongozi katika majadiliano mjini Libreville GabonPicha: dapd

Waziri  mkuu atimuliwa

Amri  tofauti inaondoa  uteuzi  wa  Faustin Archange Touadera, ambaye  amekuwa  waziri  mkuu  tangu  mwaka  2008. Chini  ya makubaliano  ya  amani , serikali  mpya  itaongozwa na  mjumbe kutoka  upinzani  wa  kisiasa  na kuielekeza   nchi  hiyo  katika uchaguzi  wa  bunge   katika  muda  wa  miezi  12 ili  kuchukua nafasi  ya  bunge  la  sasa, ambalo  linadhibitiwa  na  washirika  wa rais Francois Bozize.

Kwa  upande  mwingine , waasi  wamekubali  kusitisha  mapigano, na  kuondoa  kitisho  kikubwa  muongo  wa  Bozize  kuwapo madarakani  katika  nchi  hiyo yenye  utajiri  mkubwa  wa  madini, ambayo  ni  koloni  la  zamani  la  Ufaransa  na  kumruhusu  kumaliza kipindi  chake  cha  sasa  madarakani, ambacho  kinamalizika mwaka  2016.

The Central African Republic's President Francois Bozize looks on as he gives a press conference, on January 8, 2013 at the presidential palace in Bangui. Bozize refused on January 8 to discuss resigning at upcoming peace talks with rebels who have stormed across the country and seized several key towns. AFP PHOTO/ SIA KAMBOU (Photo credit should read SIA KAMBOU/AFP/Getty Images)
Rais wa jamhuri ya Afrika ya kati Francois BozizePicha: AFP/Getty Images

Waasi  waonya

Hata  hivyo , waasi  wamesema  kuwa  wanaweza  kuchukua  tena silaha  iwapo  serikali  itashindwa  kutimiza orodha  ya  masharti  yao katika  makubaliano  hayo, ikiwa  ni  pamoja  na  kuwaacha  huru wafungwa  wote  wa  kisiasa  na  kuondoa  majeshi karibu  yote  ya kigeni  yaliyoletwa  ili  kuliimarisha  jeshi  la  nchi  hiyo.

Seleka , muungano  wa  makundi  matano  tofauti  ya  waasi, yameanza  mapigano  mapema  mwezi  wa  Desemba, wakimshutumu  rais Bozize kwa  kupuuzia  makubaliano   ya  amani yaliyofikiwa  mwaka  2007  ambayo  yaliahidi  kutoa  ajira  na  fedha kwa  wapiganaji  ambao  wameweka  silaha  zao  chini.

Chadian President Idriss Deby Itno speaks to the press after meeting with French President Nicolas Sarkozy at Elysee Palace in Paris, France, 19 July 2007. Mr. Sarkozy received Idriss Deby Itno, who is on an official visit to France. Foto: EPA/HORACIO VILLALOBOS +++(c) dpa - Report+++
Rais wa Chad Idriss Dedy ItnoPicha: picture-alliance/dpa

Nchi  za  Afrika  ikiwa  ni  pamoja  na  Chad, Gabon, Cameroon  na Congo  zimeweka  maelfu  ya  wanajeshi  wao  kulisaidia  jeshi  la rais Bozize baada  ya  kushindwa  mara  kadha  na  kulilazimisha jeshi  hilo  kurejea  nyuma  karibu  kilometa  75 karibu  na  mji  mkuu Bangui.

Waasi  hapo  mapema  walisisitiza  kuwa  kujiuzulu  kwa  Bozize  ni moja  kati  ya  masharti  yao  kwa  ajili  ya  amani  na  kwamba  rais huyo  ambaye  ametwaa  madaraka  katika  mapinduzi  ya  mwaka 2003  yaliyoungwa  mkono  na  Chad, analazimika  kufikishwa  katika mahakama  ya  kimataifa  ya  uhalifu.

Rais  wa  chad Idriss Deby, ambaye  amehudhuria sherehe  za  utiaji saini  makubaliano  ya  amani , amesema  kuwa  makubaliano  hayo yanaonesha  maridhio mazuri.

Mwandishi : Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Iddi Ssessanga