1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika ya kusini yaweza kujihisi mshindi kwa maandalizi safi Kombe la dunia

Sekione Kitojo12 Julai 2010

Baada ya wiki nne za heka heka za fainali za kombe la dunia katika ardhi ya bara la Afrika, tunaweza kusema Afrika ya kusini imetumia vyema nasafi yake.

https://p.dw.com/p/OGlR
Mwamuzi Carlos Batres, kutoka Guatemala, kati, akimwonyesha kadi ya njano Gerard Pique, wa Hispania. Maamuzi kadha ya waamuzi yalilalamikiwa katika fainali hizi.Picha: AP

Baada ya wiki nne za heka heka za kandanda la kuwania kombe la dunia katika ardhi ya Afrika, tunaweza kusema , Afrika ya kusini imetumia vyema nafasi hii. Kimchezo hata hivyo shauku bado inaendelea.

Kama rais wa shirikisho la kandanda dunia FIFA, Joseph Blatter, alivyopata upinzani mkubwa dhidi ya kuyapeleka mashindano ya fainali za kombe la dunia katika bara la Afrika , wengi walitia shaka. Mparaganyiko wa usafiri uliokuwa ukitarajiwa haukuwapo, maeneo ya kuishi wageni, kama hoteli na kadhalika kwa mtazamo wa wengi hali ilikuwa nzuri kabisa, na uhalifu dhidi ya maafisa ama watu waliokuja kuangalia mashindano haukuonekana kabisa. Na viwanja vilikuwa safi kabisa, na hilo lilionekana hata kabla ya firimbi ya kuanzisha mashindano hayo kulia. Kwa hiyo Afrika kusini inaweza kujihisi kama mshindi wa kombe la dunia, kama duniani ilivyothibitisha , kwamba ilifanikiwa kufanya matayarisho makubwa kama hayo. Kwamba Afrika kusini na bara zima la Afrika kwa jumla linaweza kwa baadaye kufaidika na hali hiyo, hilo linabaki suala la kungoja na kuona. Kitu kidogo tu ambacho kilionekana kupunguza hali ya shauku, inapatikana katika yale matarumbeta ya vuvuzela viwanjani, ambayo yamekuwa yakimeza sauti zilizozoeleka za kupigwa mpira uwanjani , na kukandamiza sauti za mashabiki wanaoimba nyimbo za kuishabikia timu yao, na hii ilionekana kuwakera mashabiki wengi duniani. Na shangwe katika nchi nzima, kama ilivyokuwa katika fainali za kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani, mashabiki wengi waliotembelea nchi hiyo hawakuipata.

Kwa upande wa nani anaweza kuwekwa katika kiwango cha ushindi katika FIFA, Joseph Blatter anastahili pongezi, licha ya kuwa mtu anaweza hilo kulipinga. Mara nyingi shirikisho hilo la kandanda limekuwa likitoa picha isiyo nzuri.Hata katika uuzaji wao wa tiketi za mchezo, utaratibu haukuweza kufanyakazi vizuri, kama ilivyoonyeshwa na viti vilivyowazi katika viwanja. Pia maamuzi kadha ya marefa hayakuenda sambamba na uwezo wao . Na katika madai ya kutumiwa kwa vifaa vya teknolojia kusaidia kusahihisha makosa yao wameonyesha hali ya kuwapo katika mbinyo makali na majibu yao hayaridhishi. Hali ya ung'ang'anizi, kwa maslahi ya kiuchumi ya FIFA dhidi ya wafanyabiasha wadogo yalisisitizwa bila huruma, hali iliyowasikitisha wengi. Kwa jumla FIFA katika fainali hizi za Afrika kusini imethibitisha kila aina ya ukosoaji kwamba kunahaja ya kulifanyia mageuzi makubwa shirika hilo.

Kimchezo fainali hizi za Afrika kusini za kombe la dunia hazikutoa kitu kipya, kwa kuwa hadi katika robo fainali kumekuwa na michezo mibovu mingi. Na mwisho ni timu mbili tu , ambazo zimefurahisha na kujia hamasa , Uhispania , ambayo katika miaka ya hivi karibuni imefanikiwa kutengeneza timu inayocheza pasi safi fupi fupi, pamoja na Ujerumani ambayo imeonyesha kandanda safi la kushambulia.Masuala mawili lakini hata hivyo yamejitokeza katika fainali hizi. Enzi za wachezaji nyota katika kandanda zimepitwa na wakati, na timu kwa jumla kama nyota ya mchezo inaendelea kung'ara. Binafsi kuwa na nyota wawili ama watatu katika timu haisaidii kushinda mchezo, iwapo timu hiyo haifanyikazi kama timu. Pia hakuna tofauti tena inayothibitika kati ya timu inayolinda lango lake zaidi na ushambuliaji, kila mmoja anapaswa kuwa na uwezo na kuuonyesha.

Bara la Afrika halikuweza kutumia nafasi ya fainali hizi kufanyika katika ardhi yake.Ghana ilifikia tu robo fainali, ilikuwa hata hivyo timu pekee kati ya timu sita , ambayo imeweza kunusurika katika duru ya kwanza.Mafanikio hayo yalikuwa madogo sana ukilinganisha na matarajio yaliyokuwapo. Ilionekana hadi katika robo fainali kuwa timu za America ya kusini zitatamakali katika fainali hizi, lakini mwishoni timu ya bara la Ulaya zilikalia nafasi tatu. Na hii ni mbali ya timu kama Italia, Ufaransa na Uingereza timu tatu ambazo hazikuwa katika kiwango chake cha kawaida na zinahitaji kujengwa upya. Na hii inawezekana ikitiliwa maanani kuwa kuna miaka minne mbele kabla ya fainali nyingine zitakazofanyika katika bara la Amerika ambako Brazil na Argentina pia zinapaswa kuonyesha kile walichokitayarisha.

Mwandishi : van Kann , Wolfgang / ZR / Kitojo Sekione.

Mhariri: Abdul-Rahman