1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali za Afrika zatakiwa kuongeza uzalishaji wa umeme.

10 Juni 2015

Jopo la Maafisa wa ngazi ya juu limesema Serikali za Afrika zinapaswa kuongeza uzalishaji wa umeme mara 10 kwa ajili ya kuwapa watu wake wote mahitaji ya umeme hadi ifikapo mwaka 2030.

https://p.dw.com/p/1Fegt
Hinkley Point Atomkraftwerk in England
Picha: Getty Images

Theluthi mbili ya Waafrika karibu milioni 621 wanaishi bila umeme, hali ambayo ni mbaya kutokana na ongezeko la idadi ya watu, ilisema ripoti ya kila mwaka kutoka kwa wanachama 10 wa Jopo la maendeleo ya Afrika, chini ya uenyekiti wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.

Asilimia 80 ya Waafrika kupika kwa kutumia nishati itokanayo na mimea hasa kuni na mkaa na watu wapatao 600,000 wanakufa kila mwaka kutokana na uchafuzi wa hewa ya ndani, ripoti alisema.

Kuziba pengo la nishati,Mataifa ya Afrika hayana haja ya kugeukia teknologia chafu iliyopitwa na wakati, Annan aliandika katika utangulizi.

Jopo la Maendeleo ya Afrika linakuza maendeleo endelevu, na ikiwa pamoja na mwanamuziki wa Ireland na mwanakampeni Bob Geldof, aliyekuwa Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo na mtetezi wa haki Graça Machel, ambaye ni mjane wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

Ripoti ya mwaka 2015 imeweka lawama nyingi kutokana na mapungufu nishati barani Afrika mapungufu juu ya utawala mbovu wa madaraka, mara nyingi kutazamwa kama chombo cha rushwa na upendeleo wa kisiasa.

Serikali za Afrika hazijalipa umuhimu wa kutosha suala la utoaji wa nishati kwa gharama nafuu, na kuacha baadhi ya watu maskini duniani kulipa bei kubwa kwa nishati ikilinganishwa na watumiaji matajiri, ilisema ripoti hiyo.

Madame Graça Machel
Mtetezi wa Haki Graça Machel.Picha: Ismael Miquidade

Kaya zinaishi chini ya dola 2.50 kwa siku na kutumia karibu dola 10 kwa kilowatt kwa saa (kWh) kwa ajili ya vyanzo mbalimbali vya taa, wakati wastani wa gharama kwa ajili ya umeme ni dola 0.12 kilowatt nchini Marekani na dola 0.15 kilowatt nchini Uingereza.

Sekta za nishati barani Afrika zinahitaji uwekezaji wa karibu dola bilioni 55 kwa mwaka hadi 2030 kwa ajili ya kuweka nguvu ya mapungufu na kutoa huduma ya umeme kwa kila mtu, ilisema ripoti.

Sehemu kubwa ya fedha hizo kwa Serikali za Afrika zinaweza kupatikana kwa kuongeza ukusanyaji wa kodi, kuondoa rushwa, na kusitisha ruzuku zisizo na faida, kuzuia uhamisho wa fedha haramu.

Jumuiya ya kimataifa inapaswa pia kuchangia misaada na
mikopo nafuu kwa ajili ya kuunga mkono uwekezaji ambao kutoa nishati ya kisasa kwa wale wasiokuwa nayo, iliongeza.

Caroline Kende-Robb, mkurugenzi mtendaji wa Jopo, alisema sehemu kubwa ya miundombinu ya nishati Afrika bado haijajengwa, na bara liwanaweza kunufaika kwa kuchagua nishati safi kwa vyanzo kama jua na umeme wa maji, na kufunga mitambo midogo ya kuleta nishati ya umeme.

Sera ya Nishati inatakiwa kuamuliwa sasa kwa ajili ya miaka 15 hadi 20 ijayo. Hii ndiyo sababu Waafrika wanasema, 'Hii ni nafasi yetu ya kufanya mambo kwa njia tofauti, '" Caroline aliliambia shirika la habari la Reuters.

Ethiopia, Ghana, Kenya, Nigeria na Afrika Kusini tayari zimejenga mitambo mikubwa kwa ajili ya matumizi ya nishati mbadala, Ripoti alibainisha.

Ripoti ilitowa wito kwa nchi zilizoendelea kuongeza mipango ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kabla ya kufikia mkataba mpya wa kimataifa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi utakaofanyika mwezi Desemba.

Ripoti ya Jopo la Maendeleo ya Afrika ilisema nchi za G20 lazima ziweke ratiba juu ya kuondoa ruzuku zinazowekwa kufidia nishati , ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku ruzuku kwa ajili ya kufanyia uchunguzi na uzalishaji hadi mwaka 2018.

Mhandishi:Salma Mkalibala/RTRE

Mhariri:Yusuf Saumu