1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajali ya treni nchini Kongo

P.Martin3 Agosti 2007

Hadi watu 100 wamefariki dunia katika ajali ya treni iliyotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/CB2G

Kwa mujibu wa Waziri wa Habari wa kongo,Toussant Tshilombo,zaidi ya watu 200 vile vile wamejeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea kama kilomita 200 kaskazini-magharibi ya Kananga,ulio mji mkuu wa Wilaya ya Kasai ya Magharibi.

Vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa viliopo nchini Kongo,vimepeleka helikopta na matabibu katika eneo la ajali,kuwasaidia maafisa na wanajeshi wa Kongo katika kazi za uokozi.