1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al-Bashir afikishwa mahakamani mjini Khartoum

Sudi Mnette
21 Julai 2020

Rais aliyeondolewa madarakani nchini Sudan Omar al-Bashir  pamoja na baadhi ya  washirika  wake wa zamani  amefikishwa mahakamani leo  mjini  Khartoum.

https://p.dw.com/p/3feL6

Omar al-Bashir  pamoja anakikabiliwa  na  mashitaka  ya kuongoza  mapinduzi ya kijeshi  yaliyomuingiza madarakni  miaka 31 iliyopita. Mahakama  nchini Sudan tayari imemhukumu  al-Bashir kifungo cha miaka  miwili mwezi Desemba kwa  mashitaka ya rushwa. Pia  anakabiliowa na kesi na uchunguzi kuhusiana na mauaji ya waandamanaji.

Televisheni ya taifa iliripoti ufunguzi wa kesi hiyo katika mahakama  mjini  Khartoum bila ya  kumuonesha  al-Bashir, ambaye  amefungwa  tangu  alipoondolewa madarakani  Aprili mwaka jana kufuatia maandamano makubwa dhidi ya utawala wake wa miaka  30.

Soma zaidi: Sudan yaadhimisha mwaka mmoja wa mapinduzi dhidi ya Bashir

Al-Bashir amefikishwa mahakamani  katika  mji  mkuu, Khartoum leo  kukabiliana  na  mashitaka  ya kwenda kinyume  na  katiba, kukiuka sheria ya majeshi pamoja na uasi, Al-Moez Hadra, mmoja  kati ya kundi  la  mawakili ambao  wamefungua  mashitaka  ya uhalifu aliliambia shirika  la  habari  la  Ujerumani  DPA.

Sudan Khartum | Prozess & Urteil Omar al-Baschir, ehemaliger Präsident
Picha: picture-alliance/Anadolu Agency/M. Hajaj