1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al Qaeda yadai kuushambulia ubalozi wa Israel nchini Mauritania

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1jX

Kundi la Al Qaeda limedai kuhusika na shambulio dhidi ya ubalozi wa Israel mjini Nouakchott nchini Mauratania.

Televisheni ya Al Jazeera yenye makao yake makuu nchini Qatar imetangaza madai hayo ya kundi hilo bila kutoa taarifa zaidi.

Watu watatu waliokuwa wamejihami na bunduki waliufyatulia risasi ubalozi wa Israel nchini Mauritania juzi Ijumaa kabla kutoroka.

Hakuna mfanyakazi yeyote wa ubalozi huo aliyejeruhiwa lakini raia watatu wa Ufaransa waliokuwa nje ya klabu moja iliyo mita kadha kutoka ubalozi huo, walipata majeraha ya risasi.