1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al-Shabaab yawashambulia AMISOM

Daniel Gakuba
25 Oktoba 2016

Al-Shabaab inasema iliamuru mashambulizi ya kujitoa muhanga ya mshambuliaji aliyeliripua lori alilokuwa akiliendesha katika kituo cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika katikati mwa Somalia.

https://p.dw.com/p/2RgvT
Somalia al-Shabaab Kämpfer
Picha: picture alliance/AP Photo/M. Sheikh Nor

Mshambuliaji huo aliripua lori lake kwenye lango la kambi katika mji wa Beledweyne, wanakoishi wanajeshi kutoka Djibouti.

Msemaji wa kijeshi wa al-Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Musab, amesema wanajeshi wea Djibouti wamelengwa, kama kisasi vitendo vinavyokiuka madili, na mauaji vilivyofanywa na wanajeshi hao.

Umoja wa Afrika baadaye ulituma ujumbe kupitia mtandao wa Twitter, ukisema washambuliaji wapatao 10 wameuawa wote.

Rais Hassan Sheikh Mahamoud wa Somalia ameyalaani mashambuliuzi hayo, akisema wale aliowaita maadui wa amani walikuwa wakiazimia kusababisha mtafaruku ndani ya nchi yake.

Licha ya kunyang'anywa ngome zake nyingi, kundi la al-Shabab ambalo lina mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida, limekuwa likiendelea kuvishambulia vituo vya Umoja wa Afrika na vya serikali ya Somalia.