1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al- Sisi ashinda kwa kujipatia asilimia 92

Zainab Aziz
29 Machi 2018

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amechaguliwa tena kuiongoza nchi yake kwa muhula wa pili. Kiongozi huyo amechaguliwa kwa asilimia 92 ya kura kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa Alhamisi,

https://p.dw.com/p/2vDLm
Ägypten Präsident Abdel Fattah Al-Sisi
Picha: picture-alliance/dpa/K. Elfiqi

Kwa mujibu wa magazeti yanayomilikiwa na serikali ya Al-Ahram na Akhbar el-Youm, pamoja na shirika la habari la MENA, watu milioni 23 walipiga kura katika kipindi cha siku tatu zilizomalizika siku ya Jumatano, kati ya jumla ya watu milioni 60 waliorodheshwa kwenye daftari la wapiga kura.

Karatasi za kupigia kur
Karatasi za kupigia kuraPicha: picture-alliance/NurPhoto/F. El-Geziry

Kulingana na Al-Ahram, kura hizo milioni 23 zilizopigwa, kura milioni mbili ziliharibika kutokana na wapiga kura kuingiza majina ya wagombea ambao hawakuwa miongoni mwa wagombea wawili waliothibitishwa.

Mpinzani wa pekee wa al-Sisi alikuwa Moussa Mostafa Moussa asiyejulikana sana, na ambaye anamuunga mkono rais Abdel Fattah al-Sisi, Mostafa Moussa  alijiandikisha muda mfupi kabla ya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi, na hivyo kuuokoa uchaguzi huo ambao ungelikuwa ni sawa na  mbio za farasi mmoja. Wapinzani wengine, wenye uzito walitengwa na wengine waliwekwa kizuizini.

Rais wa Misri Abdel fatah al-Sisi akipiga kura yake
Rais wa Misri Abdel fatah al-Sisi akipiga kura yakePicha: Reuters/The Egyptian Presidency

Abdel Fatah al-Sisi, aliyekuwa mkuu wa jeshi alimwondoa madarakani rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa Mohamed Morsi baada ya kufanyika maandamano makubwa ya mwaka 2013. Al- Sisi alishinda muhula wake wa kwanza mwaka 2014 kwa kupata asilimia 96.9 ya kura. Kuondolewa kwa Morsi kulisababisha uharibifu mbaya, mamia ya  Waislamu wenye msimamo mkali waliuwawa.

Kukamatwa kwa wafuasi wa Morsi kulienea kwa kuwa wanaharakati waliokuwa na mtazamo wa kati pamoja na wale waliolemea mrengo wa kushoto wote walikumbwa na kamatakamata hiyo.

Asilimia 47 katika uchaguzi wa mwaka huo ilikuwa kubwa kuliko asilimia 40 ya mwaka huu licha ya miito kutoka kwa Waziri Mkuu Sherif Ismail kwa wapiga kura kwamba wajitoke kwa wingi kutekeleza uzalendo wao.

Tume ya uchaguzi ya nchini Misri imeonya kwamba wale ambao hawataweza kuonyesha sababu nzuri iliyowafanya wasishiriki kwenye uchaguzi wanaweza kukabiliwa na faini ya hadi pauni 500 za Misri sawa na euro 22.

Katika mkutano na waandidishi wa habari, afisa wa tume ya uchaguzi, Mahmud al-Sherif, amesema hakukuwepo na ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi nchini Misri.Vikundi vya upinzani vilitoa miito ya kususia uchaguzi walioufananisha na sura ya jengo. Hakukuwepo na mijadala iliyowahusisha wagombea wa urais na al -Sisi mwenyewe hakuonekana katika matukio yoyote ya kampeni rasmi, ingawa mara kwa mara alizungumza katika sherehe kadhaa.

Mabango ya kumpongeza al- Sisi
Mabango ya kumpongeza al- Sisi Picha: Reuters

Katika mahojiano kabla ya zoezi la kupiga kura, al - Sisi aliwataka Wamisri wajitokeze kwa wingi zaidi,siku ya kupiga kura. Miji ya Misri, hasa jiji la Cairo, imejaa mabango yanayomwonyesha al -Sisi pamoja na ujumbe wa kumpongeza kutoka kwa wamiliki wa biashara. Mabango kama hayo ya kumuunga mkono  Moussa Mostafa Moussa mwenye umri wa miaka 65, hayaonekani kwa wingi. Rais Abdel fatah al- Sisi ameanzisha mpango wa mageuzi magumu ya kiuchumi ambao umepokelewa vyema na wawekezaji wa kigeni lakini umempunguzia umaarufu wake nyumbani.

Mwandishi: Zainab Aziz/AFPE

Mhariri:Yusuf Saumu