1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Alexei Navalny atoka hospitali ya Berlin

Josephat Charo
23 Septemba 2020

Navalny amekuwa Berlin siku mbili tangu alipougua tarehe 20 mwezi Agosti mwaka huu.

https://p.dw.com/p/3irwi
Berlin Charite Alexei Navalny Instagram Post
Picha: Alexey Navalny/Instagram

Kiongozi wa upinzani wa Urusi, Alexei Navalny, ametoka hospitali baada ya kulazwa kwa siku 32. Hospitali ya Charite mjini Berlin iliyokuwa ikimhudumia kiongozi huyo ambaye mataifa ya magharibi yanaamini alitiliwa simu ya kiwango cha vita aina ya Novichok, imetangaza leo asubuhi.

"Kwa kuzingatia maendeleo ya mgonjwa katika matibabu na hali yake ya sasa, matabibu wanaomhudumia wanaamini inawezekana akapona kabisa," taarifa ya Charite imesema. Hata hivyo hospitali hiyo imesema ni mapema mno kutathmini athari za muda mrefu za sumu aliyotiliwa.

Navalny, mpinzani mashuhuri na wazi wa rais wa Urusi, Vladimir Putin, alisafirishwa Ujerumani siku mbili baada ya kuugua tarehe 20 Agosti mwaka huu alipokuwa katika safari ya ndege nchini Urusi. Wataalamu wa silaha za sumu wa Ujerumani walibaini kuwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 44 alitiliwa sumu ya mishipa ya enzi ya zamani ya muungano wa Sovieti. Ugunduzi huo uliifanya serikali ya Ujerumani mjini Berlin kuitaka Urusi ichunguze kisa hicho. 

Wanachama wa timu ya Navalny waliutuhumu utawala wa Kremlin kwa kuhusika kumtilia sumu kiongozi huyo wa upinzani, lakini maafisa wa Urusi wameyapinga vikali madai hayo. Utawala wa Kremlin umepuuzilia mbali miito ya kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, na viongozi wengine kujiu maswali kuhusu kutiliwa sumu Navalny.

(afp, ap)