1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria na Desemba 11

12 Desemba 2007

Algeria imekua ikiteseka na tarehe 11

https://p.dw.com/p/CabH
Hujuma AlgiersPicha: AP

Wakati Marekani imengiwa na kiwewe cha Septemba 11, waalgeria,waoanesha jiinamizi lao ni kila tarehe 11 ya mwezi wowote:Mabomu 2 yaliripuka jana Desemba 11 mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria na kuua si chini ya watu 62. Hii yabainisha magaidi wameichagua tarehe 11 ya mwezi kuhujumu.Jukumu la shambulio la jana limebebwa na kikundi kinachojiita „Al Qaeda ya eneo l la maghreb“.

Hujuma kali iliofanywa Spain,ilitokea Machi 11.Tawi hili la Al Qaeda la maghareb limeshafanya hujuma 3 tarehe hii ya 11 nchini Algerria pekee.

Walihujumu kwanza makao makuu ya serikali mjini Algiers ,April 11 mwaka huu na kuua watu 33.Miezi 3 baadae tareehe sawa na hiyo, wakaripua kambi ya wanajeshi wa serikali ya Lakhdaria,mashariki mwa Algeria na kuwaua wanajeshi 10. Shambulio la 3 ni la jana.

Uchambuzi wa Peter Philipp unaotoa mwangaza juu chanzi cha hujuma hizi mnasimuliwa sasa na Ramadhan Ali:

Mkuu wa nadharia wa mtandao wa „Al Qaeda „ Ayman Al Zawahiri, alitangaza risala yake binafsi mapema mwaka huu ambamo alikaribisha mikono miwili kuasisiwa kwa tawi la Al Qaeda la eneo la kiislamu la Maghreb au afrika ya kaskazini.

Alisema wakati ule kwamba hatua hiyo itaiumiza kichwa serikali ya Algeria.

Kigogo hicho nyuma ya Osama Bin Laden hakuacha hapo shaka shaka zozote kwamba angekaribisha matawi zaidi sawa na hilo katika nbchi nyengine za Maghreb-Afrika ya kaskazini.Kwani, matawi kama hayo kama mfano wa Algeria ulivyoonesha, hayahitaji kuongozwa kutoka shina moja.Na kabisa sio tena kutoka mpakani mwa Pakistan na Afghanistan.

Hujuma zilizotokea katika nchi za Maghreb za Morocco,Tunesia na mara kwa mara algeria kwenyewe chanzo chake na mizizi yake ya fitina kwa sehemu kubwa imeota huko huko Maghreb.

Hasa nchini Algeria kuna desturi ndefu ya mawasiliano na uongozi wa Al Qaeda-wafuasi wa kiislamu wa nadharia ya ‚Salafist“ ambao wana mafungamano na wenzao wa Misri waliounda shina la Mujahiddin.Ni kundi hilo lililiohamia Afghanistan ili kuwatimua warusi.Baada warusi kuihama Afghanistan 1989, wengi wao walirudi makwao na kujaribu kuunda dola za kiislamu nchini mwao.

Misri na Algeria zilianza kujionea kipindi cha hujuma kali za kigaidi huko nguvu za dola nazo zikijibisha mashambulio dhidi yao.

Nchini Algeria, hujuma zilichukua sura mbaya zaidi na kupelekea jeshi hapo 1992 kubatilisha uchaguzi ambao ukielekeza ushindi wa vyama vya kiislamu.

Baadhi ya viongozi wa vyama hivyo vya kiislamu vilivyokuwa vinaelekea ushindi wakakamatwa na kutiwa korokoroni,wengine wakakimbilia ngambo kuishi uhamishoni na kuakaanza vita vikali vya kienyeji vya umwagaji damu-vita ambavyo mnamo muda wa miaka 10 vimechukua maisha ya hadi watu 150.000.

Aliposhika madaraka hapo 1999, rais Abdelaziz Bouteflika , alitangaza shabaha ya kurejesha nchini Algeria suluhu na maskizano.Akaregeza kamba na kuwatoa baadhi ya wafuasi wenye itikadi kali ya kiislamu korokoroni.Bouteflika akaitisha kura ya maoni ili wananchi waidhinishe msamaha .Matokeo yake leo si nadra kwa majirani wauaji na waliouliwa jamaya zao wanaishi pamoja mtaa mmoja.

Shabaha za hujuma za magaidi ni taasisi za serikali kama vile wizara ya ndani hapo septemba au hata wanasiasa wa Algeria:hujuma kuwaua hata rais Abdelaziz Bouteflika na waziri wake mkuu Abdelazizi Belhadem.

Kwa jicho hili hata mabingwa kutoka nje –warusi,wamarekani na wafaransa wameanguka mateka.Maana ya hujuma hizi:Algerias irudi kutengwa na katika hali za shida kubwa, mtandao wa maghreb wa Al Qaeda upate chipukizi wapya.

Ndio maana Al Zawahir, tayari mwanzoni mwa mwaka huu aliitisha wafaransa na wamarekani watimuliwe nje ya Algeria.