1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Kiongozi wa kundi la kiislamu alaani uhusiano baina ya Algeria na Ufaransa

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjx

Kiongozi wa kundi la mahubiri na mapambano la Salafist nchini Algeria, GSPC, lenye mafungamano na kundi la al Qaeda, amelaani vikali juhudi zinazofanywa kuboresha uhusiano baina ya Algeria na Ufaransa.

Abu Musab Abdul Wadud, amepuuza juhudi za kusaini mkataba wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili akisema bado kuna ukuta wa mafuvu ya vichwa na vipande vya maiti pamoja na bahari ya machozi na damu kati ya Ufaransa na Algeria.

Aidha kiongozi huyo amesema kwenye ujumbe wake uliotumwa kwenye tovuti inayotumiwa na wanamgambo wa kiislamu, kwamba Uislamu halisi unakataza urafiki na makafiri.

Ujumbe huo ulitumwa wakati rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, alipokutana na rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, kujadili njia za kuwa na ushirikiano wa karibu kati ya nchi zao.

Rais Sarkozy anaendelea na ziara yake nchini Algeria ikiwa ni ziara yake kwanza nje ya Ulaya tangu alipochaguliwa kuingoza Ufaransa mnamo mwezi Mei.