1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amerika ya Kusini itamudu kukabiliana na mgogoro wa Kiuchumi

sudi mnete15 Aprili 2009

Mwenyekiti wa Benki ya lloyds amesema nchi za Marekani ya Kusini zipo katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi.

https://p.dw.com/p/HXEZ
Rais Lula Ignacio da Silva wa BrasilPicha: AP



Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Reo De Jeneiro Peter Levene amesema ni bahati kwa wakazi wa eneo hilo kwa sababu kiini cha mgogoro wa kiuchumi ni mabenki.


Aidha amesema ni dhahiri kwamba nchi za Amerika ya Kusini hazijahathirika sana kama ilivyo kwa nchi za Marekani,Ulaya na nyingine za Bara la Asia.


Kiongozi hiyo wa Benki ya Uingereza akiwa miongoni mwa watu wanaoudhuria Kongamano la Kimataifa la Kiuchumi lililoanza jana nchini Brazil.


Benki ya Uingereza ni miongoni taasisi zilizokuwa na soko kubwa la kutoa huduma za bima Duniani.


William Rhodes ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara wa Marekani ni miongoni mwa wadau wa mkutano huo ambaye pamoja na mambo mengine anasema utaleta tija kwa Wananchi wa Kanda hiyo.


''Mfumo wa mabenki katika mataifa ya Amerika ya Kusini iko imara ninavyojua mimi,hilo mosi.Pili ukitathmini viwango vya fedha zilizohifadhiwa za mabenki kuu ya eneo hilo utaona kwamba yako katika kiwango maalum.Tatu tumeshuhudia maendeleo mengi katika sekta ya kuimarisha taasisi za fedha katika kipindi cha miaka michache iliyopita''


Mkutano huo wa siku tatu unaowakutanisha wachumi mbalimbali pamoja na mambo mengine una lengo la kujadili majukumu ya Kanda hiyo katika kujikwamua na mgogoro wa kiuchumi.


Hatua hiyo ya kufanyika kwa mkutano huo inatokana na kumalizika kwa Mkutano wa nchi Tajiri zilizoendelea kiviwanda Duniani G20 huko London ambao umetoa fursa ya kuendelea kwa mjadala wa kikanda.


Mmoja kati ya Waratibu wa Kongamano hilo Emilio Lozoya amesema katika mkutano huo kunatarajiwa kuwepo kwa mijadala itakayoibua mipango madhubuti ambayo itaelekeza namna ya kukabiliabna na mgogoro wa kiuchumi.


Pamoja na kuwepo kwa hotuba ya ufunguzi itakayotolewa na Rais Lula da Silva wazungumzaji wengine ni Marais Alvaro Uribe wa Colombia,Leonel Fernandez wa Jamhuri ya Dominica.


Inakadiliwa zaidi ya watu 500 kutoka nchi 37 wanaudhuria mkutano huo wakiwemo Wanasiasa,Wachumi na Mashirika mengine.


Ukiacha mjadala wa namna ya kukabilana na mgogoro wa kiuchumi katika kanda hiyo mambo mengine yatakayojadiliwa ni kuhimarisha uhusiano wa kikanda,mipango endelevu na utunzaji wa mazingira.


Wapembuzi wa mambo wamesema Kongamano hilo litawapa Marais Rais Lula da Silva na Fernendez kuwa na sera ya pamoja watakayoiwasilisha katika katika Kongamano la Mabara ya Marekani ya Kusini na Kaskazini litakalofanyika Trinidad na Tobago ijumaa hii.


Kwa mujibu wa Ripoti ya wiki iliyopita ya Tume ya Uchumi ya Amerika ya Kusini EACLA nchi za ukanda huo zitarajiea athari za mgogoro wa kiuchumi.


Mwandishi: Sudi Mnette/RTRE

Mhariri:M.Abdul-Rahman