1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amman. Mawaziri wa mambo ya kigeni wakutana Jordan.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCne

Waziri mkuu wa Jordan Marouf Bakhit amefungua kikao kwa ajili ya mkutano utakazungumzia masuala ya mikutano ijayo kwa kusema kuwa kutanzua kwa mgogoro kati ya mataifa ya Kiarabu na Israel ni muhimu ili kuweza kufanikisha mageuzi katika mashariki ya kati.

Bwana Bakhit amesema , inasikitisha kuona kuwa eneo hili linasumbuliwa na migogoro kadha na hali ya wasi wasi pamoja na kutokuwapo ufumbuzi wa haraka wa mizozo hiyo hali ambayo italeta mkwamo kwa haja ya watu wa eneo hili ya mageuzi.

Mawaziri wa mataifa 38 ikiwa ni pamoja na wale wa kundi la G8 wanashiriki katika mkutano huo , ambao unatarajiwa kujadili hali ya wasi wasi katika ardhi ya Palestina , Iraq na Lebanon.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani ameueleza mkutano huo kuwa ni nafasi nzuri , kwake kutokana na kufanya mazungumzo hapo kabla katika mamlaka ya palestina , Lebanon na Israel.