1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN:Kamati ya wasomi kujadilia masuala ya waislamu yaundwa

12 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBa5

Nchi ya Jordan imeunda kamati ya wasomi 100 wa Kiislamu ili kushughulikia masuala yanayowagusa kwa karibu waislamu kote ulimwenguni.Kamati hiyo kwa jina Salam inalenga kuandaa mazingira ya majadiliano na mdahalo ili kutumia mawazo kutuliza ghasia aidha kupata ufumbuzi wa masuala nyeti.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo mvutano uliosababishwa na vibonzo vya Mtume Muhammad (S.A.W) ilidhihirisha namna Uislamu unatatizwa na uongozi usio na usomi.Kamati hiyo inapendekeza kukabiliana na matatizo au mivutano ambayo huenda yakatumiwa na waislamu wa misimamo mikali.

Kamati hiyo inaongozwa na mjombake Mfalme Abdullah wa pili Prince Hassan wa zamani.Aidha inawahusisha waislamu mashuhuri ulimwenguni akiwemo Mkurugenzi mkuu wa shirika la Kiislamu la Elimu,Sayansi na Utamaduni Abdulaaziz Othman Altwaijiri pamoja na Mawaziri wakuu wa Yemen Abdul Karim- Eryani na Haider Abubakary al Attas.-

Mwaka 2004 nchi ya Jordan ilizindua mpango kw ajina Ujumbe wa Amman unaolenga kuwahamasisha waislamu kuasi ugaidi na badala yake kutilia mkazo uvumilivu na makubaliano katika jamii.