1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM:Kesi ya Charles Taylor yaahirishwa hadi Agosti

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmU

Majaji katika Mahakama maalum ya Umoja wa mataifa kwa ajili ya Sierra Leone wanaahirisha kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili Rais wa Liberia wa zamani Charles Taylor.Kesi hiyo itasikizwa tena tarehe 20 mwezi Agosti ili kuwapa muda zaidi wa kujiandaa upande wa utetezi.

Bwana Taylor anakabiliwa na kuhusika na vitendo vya uhalifu nchini Sierra Leone vilivyosababisha vifo,ubakaji na ukatili ili kunufaika na almasi nchini humo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.Charles Taylor amesusia vikao vya mahakama tangu kesi kufunguliwa mwezi jana kwa madai kwamba hana fedha za kutosha kutafuta mawakili .

Wiki jana Jaji Julia Sebuttinde aliagiza mahakama kumwongezea mawakili wengine wane wa ziada ifikapo mwishoni mwa mwezi huu ili kuhakikisha usawa.

Bwana Taylor ambaye hafika mahakamani tnagu mwezi jana alimwachisha kazi wakili wake wakati kesi ilipofunguliwa rasmi na kusema kuwa anajitetea mwenyewe.Hata hivyo alibadili mawazo na kudai kupewa wakili hodari.

Rais huyo wa zamani wa Liberia anakanusha mashtaka 11 ya uhalifu wa kivita na uhalifu wa kikatili dhidi ya ubinadamu uliotendekea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1991 hadi 2002.