1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angela Merkel amechaguliwa kansela kwa awamu ya pili

28 Oktoba 2009

Bibi Angela Merkel leo ameidhinishwa na bunge kuwa kansela wa Ujerumani na hivyo serikali ya muungano wa vyama ndugu vya kihafidhina CDU/CSU na chama cha kiliberali FDP, inaweza kuanza kufanya kazi.

https://p.dw.com/p/KI3K
Angela Merkel (CDU, Mitte) erhält am Mittwoch (28.10.2009) im Reichstag in Berlin Beifall bei der Bekanntgabe ihrer Nominierung zur Bundeskanzlerin, neben ihr applaudieren Volker Kauder (l) und Peter Ramsauer. Merkel ist mit großer Mehrheit für eine zweite Amtszeit wiedergewählt worden. Die 55-Jährige erhielt im Bundestag in Berlin 323 von insgesamt 612 abgegebenen Stimmen. Merkel steht an der Spitze einer schwarz-gelben Koalition aus Union und FDP. Seit Oktober 2005 hatte sie zusammen mit der SPD regiert. Foto: Arno Burgi dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++
Angela Merkel(kati) akipigiwa makofi bungeni baada ya kuchaguliwa kuwa kansela kwa awamu ya pili.Picha: picture-alliance/dpa

Naam, Angela Merkel amechaguliwa tena kuwa kansela wa Ujerumani na waziri wake wa mambo ya nje ni mpya.Hiyo lakini haimaanishi kuwa kutakuwepo mabadiliko mengi kwani hakuna sekta inayopewa mwongozo na kansela kama katika sera za nje. Hilo alitambua waziri wa zamani wa mambo ya nje Steinmeier aliependelea zaidi kuwa na sera za maelewano pamoja na serikali za Beijing na Moscow. Hata hivyo, Mkataba wa Lisbon utakapoanza kutumika, sera za nje zitaongozwa zaidi na Umoja wa Ulaya kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Kwa upande mwingine, washirika wapya wa Angela Merkel ni waliberali walio maarufu kwa msimamo wao wa kupendelea kupunguza huduma za kijamii. Lakini huduma za jamii zilipinguzwa na Gerhard Schroeder aliekuwa kansela wa chama cha social demokratik kwa kiwango kikubwa kabisa katika historia ya Ujerumani kufuatia vita vikuu vya pili. Chini ya uongozi wake hata sheria za masoko ya fedha zilirekebishwa na kodi ya mapato ya wajasiriamali na wenye kupokea mishahara ya juu, ikapunguzwa.

Schroeder alichukua hatua hizo chini ya shinikizo la utandawazi huku viwanda vikihamishwa nchi za ngambo na nafasi za ajira kutoweka. Alifanikiwa kupunguza idadi ya wakosa ajira. Hata hivyo maisha ya wananchi wengi yalizidi kuwa magumu na hatimae Schroeder alipoteza madaraka yake.

Hata sera za Angela Merkel katika awamu yake ya pili madarakani, zitashawishiwa na hali ya kiuchumi na kisiasa duniani kuliko ilivyokuwa awamu iliyopita. Kwani katika kupambana na msukosuko wa uchumi na madhara yake, Merkel hana budi kukubali kuwa nchi itakuwa na deni kubwa sana. Lakini atapaswa pia kudhibiti hali ya ukosefu wa ajira unaozidi kuongezeka ili asijikute kule alikoanzia Gerhard Schroeder, lakini tofauti ni kuwa safari hii serikali imepungukiwa uwezo wa kifedha.

Kwa hivyo, mwanzoni Angela Merkel atapaswa kwenda hatua kwa hatua na sio kushikilia njia moja tu. Haijulikani vipi anatazamia kupunguza deni kubwa la serikali na idadi kubwa ya wakosa ajira miongoni mwa wale wenye elimu ya chini - sharti mojawapo la kusaidia kupunguza pengo la fedha serikalini. Ni mengi yanayongojewa na kila mmoja amekodolea macho.

Mwandishi: P.Stützle/ZPR

Mhariri:M.Abdul-Rahman