1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Mahakama Kuu yaruhusu kura ya maoni

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlT

Mahakama Kuu nchini Uturuki imeunga mkono mipango ya serikali ya kutaka kuitisha kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba.Kuambatana na mageuzi hayo,katika siku zijazo badala ya bunge ni wapiga kura watakaomchagua rais wa nchi.Uamuzi wa mahakama umeimarisha nafasi ya waziri mkuu Tayyip Erdogan na chama chake kinachopigania kuchaguliwa tena katika uchaguzi utakaofanywa tarehe 22 mwezi huu.Raia wasiotaka dini kuingilia katika uongozi wa serikali,wana hofu kuwa chama cha waziri mkuu Erdogan kitaimarisha usemi wa dini nchini humo, pindi chama hicho kitashinda uchaguzi wa rais.