1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Waasi wa Kikurd wazingirwa milimani

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Bb

Vikosi vya Uturuki vimewazingira kiasi ya waasi 100 wa Kikurd katika eneo la milimani,karibu na mpaka wa Irak.Shirika la habari la Uturuki, Anatolia limesema,wanajeshi wa Uturuki waliziba njia zinazotumiwa na wanamgambo wa chama cha Kikurd cha PKK,kurejea kwenye vituo vyao kaskazini mwa Irak baada ya kuishambulia Uturuki. Operesheni ya vikosi vya Uturuki katika eneo la Yuksekova,kusini mashariki ya Uturuki imefanywa siku moja baada ya kuuawa kwa waasi 15 wa PKK.

Wakati huo huo,serikali ya Ankara inajitayarisha kwa majadiliano muhimu pamoja na Marekani kutafuta njia ya kuutenzua mgogoro unaohusika na kambi za waasi kaskazini mwa Irak.