1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Uturuki yaonya uhusiano wake na Marekani utasambaratika ikiwa Pkk watabakia Kaskazini mwa Iraq

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BB

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema uhusiano kati ya nchi yake na Marekani utakuwa katika hali mbaya ikiwa waasi wa kikurdi wa chama PKK wataendelea kuwa kaskazini mwa Iraq.

Matamshi hayo ya bwana Erdogan yametolewa wakati ambapo anatarajiwa kukutana tarehe 5 Novemba na rais Gorge W Bush mjini Washington kuzungumzia njia za kupambana na waasi hao wa Pkk.Hata hivyo Marekani imekuwa ikiionya Uturuki juu ya kuanzisha mashambulio kaskazini mwa Iraq dhidi ya waasi hao kwa kuhofia kwamba usalama wa eneo hilo huenda ukasambaratika kama maeneo mengine ya Iraq.

Uturuki imeweka maelfu ya wanajeshi wake pamoja na vifaru,ndege za kivita na silaha nzitonzito katika eneo la mpakani na Iraq kwa ajili ya kujitaarisha na uwezekano wa kuwashambulia waasi wa Pkk kaskazini mwa Iraq.