1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Viongozi wa Irak na Uturuki wameanza mazungumzo muhimu

26 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CX

Mazungumzo muhimu kati ya Irak na Uturuki yanayojadili mkakati wa kuepusha mashambulio zaidi ndani ya mipaka ya Irak yameanza katika wizara ya mambo ya nje mjini Ankara nchini Uturuki.

Waziri wa ulinzi wa Irak na mwenzake wa usalama wa ndani wanakutana na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki na mwenzake wa mambo ya ndani.

Uturuki inasemakana kuwa imewapeleka mamia ya wanajeshi wake kwenye maeneo ya mpakani na Irak tayari kwa mashambulio dhidi ya waasi wa kikurdi wa chama cha wafanyakazi cha PKK.

Awali rais Abdullah Gul wa Uturuki alionya kuwa nchi yake haina tena subira.

Umma wa Uturuki umekuwa ukipaza sauti kwamba serikali iwachukulie hatua waasi wa Kikurdi tangu waasi hao walipowauwa askari 12 wa Uturuki katika mapigano ya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ndege za kivita za Uturuki zimefanya mashambulio kadhaa ndani ya eneo la Irak tangu tukio hilo.