1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annegret Kramp-Karrenbauer kutowania ukansela Ujerumani

Grace Kabogo
11 Februari 2020

Kiongozi wa chama cha Christian Democratic Union, CDU Annegret Kramp-Karrenbauer hatogombania kinyang'anyiro cha kumrithi Angela Merkel kuwa kansela wa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/3XXRF
Deutschland CDU-Chefin fordert von SPD und Grünen neuen Kandidaten in
Erfurt
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Kappeler

Msemaji wa chama cha CDU amesema Kramp-Karrenbauer pia atajiuzulu uenyekiti wa chama cha CDU. Kramp-Karrenbauer, mwenye umri wa miaka 57 alikuwa akipigiwa upatu kuchukua nafasi ya ukansela mwaka 2021 baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CDU mwaka 2018.

Hata hivyo, tangu wakati huo, Kramp-Karrenbauer anayejulikana kama AKK, amekumbwa na kashfa kadhaa, ikiwemo uchaguzi wa wiki iliyopita katika jimbo la Thuringia, ambapo wanachama wa CDU walipiga kura kwa kushirikiana na chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia na kinachopinga wahamiaji, AfD kumchagua waziri mkuu mpya wa jimbo hilo.

Duru zimeeleza kuwa Merkel anataka Kramp-Karrenbauer abakie kuwa waziri. Kwa sasa Kramp-Karrenbauer ni waziri wa ulinzi.