1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANTANANARIVO : Kura zaanza kuhesabiwa

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmt

Maafisa wa uchaguzi nchini Madagascar wameanza kuhesabukura kufuatia uchaguzi ambao unatazamiwa kumpa Rais anayetetea wadhifa huo tajiri mkubwa Marc Ravalomanana kipindi cha pili madarakani.

Waangalizi wa uchaguzi wanasema kituo kimoja cha kupigia kura kilifungwa wakati wapiga kura wenye hasira walipokiwasha moto lakini venginevyo uchaguzi huo ulifanyika kwa amani.

Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika tokea mgogoro wa kisiasa ulipokiweka kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe hapo mwaka 2001 na mwaka 2002.