1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANTANANARIVO:Bunge lavunjwa kisiwani Madagascar

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBek

Rais wa Madagascar Marc Ravalomanana anatetea uamuzi wake wa kuvunja bunge nchini humo kwa lengo la kupambana na umasikini ili kuimariosha utendaji kazi.Wabunge walipewa saa 48 kuhama afisi zao baada ya rais Ravalomanana kuvunja bunge wiki hii kwa madai kuwa haliwakilishi wananchi.

Wabunge hao wanafanyiwa uchunguzi kwa madai ya kuhusika na visa vya rushwa na magendo na magari yao kupekuliwa ili kutafuta komputa na vifaa vengine ambavyo huenda viliibiwa.

Hatua ya rais huyo inaungwa mkono na mahakama kuu na inatokea miezi mitano kabla muda wa muhula wa bunge kukamilika.Wabunge hao walichaguliwa mwaka 2002.Bwana Ravalomanana anatangaza tarehe 23 mwezi Septemba kama tarehe mpya ya uchaguzi wa wabunge.Bunge jipya linatarajiwa kuwa dogo zaidi likiwa na wasaidizi 127 badala ya 160 wa awali.