1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

App ya uchunguzi wa saratani ya maziwa Uganda

19 Novemba 2015

Kisa cha App ya uchunguzi wa saratani ya maziwa kinaonyesha namna uzoefu wa kimaendeleo na kivitendo, na tabia za kimataduni vinapaswa kwenda sambamba ili hatimaye kupata mafanikio katika soko.

https://p.dw.com/p/1H8wj
DW - Africa on the move
Picha: DW

Uganda: App ya uchunguzi wa saratani ya maziwa

Wakiwa na idadi kubwa ya raia wenye umri zaidi duniani, upatikanaji unaoongezeka kwa kasi zaidi wa intaneti, na kasi ya matumizi ya simu za mkononi, Waganda wameanza kukumbatia ubunifu wa teknolojia za habari na mawasiliano. Kulingana na faharasi ya ubunifu ya dunia ya mwaka 2014, Uganda ni nchi inayojifunza ubunifu, ikiwa miongoni mwa nchi zinazozipiku nyingine katika makundi yao ya kipato, zikiwa na ufanisi wa zaidi ya asilimia 10 juu kuliko kiwango chao cha pato jumla la ndani, kufuatana na viwango vya mapato. Nchi nyingine katika tabaka hili ni Kenya, Msumbiji, Rwanda, Burkina Faso na Gambia. Mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara yanachangia karibu asilimia 50 ya mataifa yanayochipukia kwa ubunifu duniani. Kulingana na mtaalamu wa teknolojia ya mawasiliano Michael Ninyitegeka, maendeleo ya ubunifu wa teknolojia ya mawasiliano yamekuwa ya mtawanyo kuliko ya kimfumo, kutokana na ukweli kwamba kuna utafiti mdogo unaofanywa na pia uwekezaji wa kimaendeleo kwa ngazi ya taifa au ya kampuni nchini humo. Kisa cha App ya uchunguzi wa saratani ya maziwa kinaonyesha namna uzoefu wa kimaendeleo na kivitendo, na tabia za kimataduni vinapaswa kwenda sambamba ili hatimaye kupata mafanikio katika soko.