1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arab League yahimiza rais achaguliwe haraka Libnan

Oummilkheir6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cl6T

Katibu mkuu wa jumuia ya nchi za kiarabu,Amr Moussa anapanga kufika ziarani mjini Beyrouth hivi karibuni,kuwasilisha mpango wa nchi za kiarabu unaohimiza kiongozi wa jeshi Michel Suleiman achaguliwe haraka kua rais wa Libnan.Akizungumza na waandishi habari mjini Cairo,Amr Moussa amesema ziara yake itafanyika siku mbili kutoka sasa.Mjini Bayrouth,kiongozi wa chama kinachodhibiti wingi wa viti bungeni,Saad Hariri ameusifu uamuzi huo na kuutaja tunanukuu kua “msimamo wa kihistoria,uliotukuka na wa kiadilifu wa nchi za kiarabu kwa mzozo wa kisiasa wa Libnan.Mwisho wa kumnukuu.Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi 22 za jumuia ya nchi za kiarabu,akiwemo pia Walid Mouallem wa Syria wamepitisha mpango wa awamu tatu kuisaidia Libnan ijikwamue toka mzozo wa kisiasa-mbaya kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipomalizika mnamo mwaka 1990.Libnan haina rais kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu hivi sasa.Baada ya kuakhirishwa mara 11,bunge la Libnan linatazamiwa kukutana tena january 12 katika juhudi za kumchagua rais mpya.Mkuu wa vikosi vya wanajeshi Jenerali Michel Suleiman ni mgombea wa maridhiano wa pande zote zinazohusika na mzozo wa Libnan.