1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Argentina yaizamisha Brazil

Aboubakary Jumaa Liongo18 Novemba 2010

Mechi za kimataifa za kirafiki zimeshuhudia vigogo, Brazil,na Uhispania vikipigwa mwereka.

https://p.dw.com/p/QCKz
Lionel Messi akipachika bao dhidi ya BraziPicha: AP

Ujerumani kwa upande wake ikichezesha kikosi cha chipukizi wengi, imetoka suluhu bin suluhu na Sweden, katika moja ya mechi za kirafiki hapo jana huko Sweden.

Lakini Uingereza ilichapwa nyumbani na Ufaransa mabao 2-1, huku bao la Lionel Messi likiizamisha Brazil huko Qatar mbele ya mahasimu wao Argentina.

Katika mechi nyingine, Ivory Coast ilichapwa ugenini na Poland mabao 3-1, huku mabingwa wa dunia Uhispania wakizabwa na Ureno mabao 4-0 mjini Lisbon..

Mwandishi:Aboubakary Liongo