1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASCHGABAT: Waziri Steinmeier ziarani Turkmenistan

2 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwm

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier hii leo anaanza ziara yake nchini Turkmenistan.Wakati wa ziara hiyo ataonana na rais Saparmurat Niyasov alieitenga nchi yake na jumuiya ya kimataifa.Serikali ya Turkmenistan inatuhumiwa kukiuka haki za binadamu na kukandamiza kila aina ya upinzani.Waziri Steinmeier wakati wa ziara yake atachunguza uwezekano wa kuwepo ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Asia ya Kati na Umoja wa Ulaya.