1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Askofu Mkuu wa Mosul atekwa nyara Irak

1 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DGEU

MOSUL:

Vikosi vya usalama vimesambazwa kila pembe katika mji wa Mosul,kaskazini mwa Irak kumsaka Askofu Mkuu wa Kikatoli wa Chaldi alietekwa nyara siku ya Ijumaa. Faraj-Faraj Rahhu ni askofu mkuu katika mji wa Mosul.Alikamatwa kufuatia mapambano ya kufyatuliwa risasi na wenzake watatu kuuawa.

Idadi fulani ya viongozi wa Kikristo wametekwa nyara nchini Irak tangu majeshi ya kigeni chini ya uongozi wa Marekani kuivamia nchi hiyo katika mwaka 2003.Baba mtakatifu Benedekit XVI amelaani utekaji nyara huo kama ni kitendo cha uovu kinachoathiri kanisa zima nchini Irak.