1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Athari za lugha za kienyeji kwenye uchaguzi wa Kenya

Admin.WagnerD5 Machi 2013

Kukihesabiwa siku chache kabla ya zoezi zima la uchaguzi mkuu kufanyika nchini Kenya, jukumu la wanahabari hasa katika vituo vinavyozungumza lugha ya mama, linapaswa kuzingatiwa kimaudhui kuepusha vurugu za uchaguzi

https://p.dw.com/p/17ncZ
PHOTO 1 - CAPTION: Dkt. Bitange Ndemo, Permanent Secretary in Ministry of Information and Communication in Kenya (LEFT) and Ms Mary Ombara wa from special committee which assessing media reports during election.
Kenya Wahlen 2013Picha: Reuben Kyama.

Wazo hilo linatokana na taarifa kwamba katika ghasia za baada ya uchaguzi miaka mitano iliyopita, redio hizo zinazozungumza lugha ya mama zilisemekana kuchangia katika ghasia hizo kwa kutoa matamshi ya chuki.

Ni kutokana na hilo ambapo kikao maalumu cha kujadili nafasi ya vyombo vya habari hasa zile zinazotangaza kwa lugha asilia kimeitishwa jijini Nairobi (28.02.2013). Mkutano huo umeitishwa na Wizara ya Habari na Mawasiliano na unawashirikisha washika dao kutoka sekta ya habari na mawasiliano na pia waakilishi kutoka tume ya uwiano na maridhiano, yaani NCIC.

Dhima ya vyombo vya habari katika uchaguzi

Waandalizi wa kikao hicho, wamesema lengo hasa ni kujadili kwa kina mchango wa vyombo vya habari katika uchaguzi ikizingatiwa kuwa vyombo vya habari vilichangia kwa kiasi kikubwa machafuko yaliyofuatia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.

Habiba Maalim, center, and other girls at Khadija Umul Mumminin girls' primary school in Mandera, northeastern Kenya listen to an English lesson broadcast on a WorldSpace satellite radio in this Wednesday, Nov. 6, 2002 photo. WorldSpace was set up by Noah Samara, an Ethiopian-American, in 1990 in a bid to help spread information in some of the world's poorest countries. (AP Photo/Karel Prinsloo)
Wanafunzi wa Kenya wakisiliza radioPicha: AP

Mary Ombara ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Kamati ya Kitaifa inayofuatilia maswala ya vyombo ya habari. Anasema mkutano ametaja umuhimu wa mkutano huo kuwa ni mjadala muhumu kuhusu ni suala nyeti la usambazaji habari za matukio "Sisi kama wizara husika tumeitisha kikao hiki ili kugusia juu ya wajibu wa wanahabari wakati wa uchaguzi na kuhakikisha kuwa wanat\umia vyombo vyao kueneza amani". Alisema Ombara

Serikali ya Kenya yajizatiti kuukabili uchochezi

Nae Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari na Mawasiliano Dkt. Bitange Ndemo, alisema serikali imeweka mikakati kabambe kukabiliana na tatizo la uchochezi miongoni mwa vyombo vya habari, hususan vile vinavyorushia matangazo kwa lugha asilia.

PHOTO 2 - CAPTION: Dr.. Bitange Ndemo, Permanent Secretary in the Ministry of Information and Communication was speaking at the meeting which discussed about the role of media in the election, was made ​​today (28/02/2013) in Nairobi Pic/ By Reuben Kyama. .
Katibu Mkuu Wizara ya Habari na Mawasiliano Kenya Bitange NdemoPicha: Reuben Kyama.

Zaidi ya watu wapatao elfu 1,300 walifariki katika vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ilhali mamia ya maelfu ya wengine waliachwa bila makao. Vyombo vya habari, hasa stesheni za redio zinazotangaza kwa lugha za asili zimelaumiwa kuhusika katika uchochezi uliopelekea vurumai hiyo.

Matukio ya uchochezi yameanza

Inaripotiwa kuwa tayari vituo viwili vya redio, wanablogu na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanachunguzwa na polisi kwa tuhuma za kueneza chuki. Dkt. Ndemo anasema kwa wakati huu serikali inapata changamoto kubwa kutokana na matumizi ya utandawazi.

Hata hivyo, Bi. Ombara anasema katika yake inalo jukumu la kuchunguza na kutoa mapendekezo endapo kutakuwepo na uchochezi wa aina yo yote kutoka kwa mashirika ya habari.

Kuna takriban vituo vya  redio 100 nchini Kenya, zikiwemo zile zinazotangaza kwa lugha za kiasili. Mtangazaji wa kituo kimoja mashuhuri nchini kenya ni miongoni mwa watuhumiwa wanaokabiliwa na mashtaka ya kujibu katika mahakama ya kimataifa ya Jinai, mjini Hague.

Mwandishi: Reuben Kyama
Mhariri: Josephat Charo