1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS:Mkasa wa Moto waendelea kuzusha hisia kali kwa wagiriki

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUY

Maafisa wa zima moto nchini Ugiriki wamefahamisha kwamba wamefanikiwa kupunguza nguvu za mioto ya porini iliyokuwa imeenea katika maeneo mengi ya nchi kwa muda wa siku sita.

Idara ya zima moto hata hivyo imesema bado kunawasiwasi na kwamba wimbi la joto lililotabiriwa kutokea mwishoni mwa juma huenda likachochea upya kuzuka mioto hiyo.Kwa sasa serikali imeanza kuangalia jinsi ya kuwasaidia waathirika wakati raia wakiandamana kupinga jinsi serikali ilivyolishughulikia suala zima la mkasa huo wa moto ambao ulisababisha kuwawa kwa zaidi ya watu

Serikali inakabiliwa na shutuma za kushindwa kukabiliana na mioto hiyo.Wiki chache zijazo raia wa Ugiriki watapiga kura katika uchaguzi wa wa mapema wa Bunge uliotishwa kabla ya kuzuka mkasa huu wa moto.