1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATLANTA: Watu takriban 20 wauwawa kwenye vimbunga

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCN8

Watu takriban 20 wameuwawa kwenye vimbunga vilivyopiga katika majimbo matatu ya kusini mwa Marekani. Maafisa wa jimbo la Alabama wamesema watu wasiopungua saba wameuwawa wakiwemo wanafunzi watano katika shule ya upili ambako wanafunzi walifunikwa na paa lililoporomoka.

Mmoja wa wanafunzi aliyeponea chupuchupu kimbunga hicho amesema waliangukiwa na paa la jengo walimokuwa.

´Kimbunga kilipiga na paa likatuangukia. Na kwa bahati nzuri paa lilijengwa na matofali ya mkaa kwa hiyo kuta hazikuanguka. Lakini hata hivyo matofali kadhaa ya nje yaliporomokea ndani na kuwaangukia baadhi ya watu waliokuwa wametuzunguka.´

Madarzeni ya watu wamejeruhiwa na kupelekwa hospitalini. Msichana wa umri wa miaka saba aliuwawa kufuatia kimbunga kikali katika jimbo la Missouri. Watu wengine watatu wameuwawa kusini mwa jimbo la Georgia.

Wakati haya yakiarifiwa watu sita wamekufa baada ya basi lililokuwa limewabeba wachezaji wa timu ya besiboli kuanguka. Duru ziansema watu wengine tisa wamejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo.