1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Atletico wanufaika na matokeo ya El Classico

24 Machi 2014

El Classico ni mechi ambayo bila shaka huzungumziwa sana kote ulimwenguni na kuzusha hisia kali, siyo kwa sababu ya ukubwa na mafanikio ya timu zote mbili tu, hapana. Yapo mengi tu....

https://p.dw.com/p/1BV3W
Classico Messi Real Madrid vs Barcelona
Picha: Reuters

Mchuano wa watani wa tangu jadi Real Madrid na Barcelona almaarufu El Classico huwa wa kipekee na kama kawaida hapo jana mashabiki wa timu zote mbili na ulimwengu kwa jumla ulishuhudia burudani kutoka ngome ya Madrid, Estadio Santiago Bernabeu.

Kama kawaida, mechi hiyo haikukosa sarakasi zake, na hata manung'uniko ya refa kuchangua katika matokeo hayo…Barca waliibuka washindi kwa kuwafunga Madrid magoli manne kwa matatu, wakati kukiwa na penalty tatu, moja ya Real na mbili za Barca…

Mchuano wa El Classico huwa kati ya Ronaldo na Messi
Mchuano wa El Classico huwa kati ya Ronaldo na MessiPicha: Reuters

ni mechi iliyokuwa na umuhimu kwa timu zote mbili na hasa Barca, lakini baada ya kipenga ya mwisho kupulizwa, ilikuwa wazi kuwa waliosherekea sana usiku kucha walikuwa ni Atletico Madrid, ambao wanaongoza msimamo wa Ligi ya Uhispania wakiwa na points 70 sawa na Real katika nafasi ya pili. Barca ni watatu na pointi 69.

Matokeo hayo yamekifanya kinyang'anyiro cha kuwania taji la msimu huu kuwa la kusisimua kabisa na tutasubiri kuona ni nani ana pumzi za kutosha kuvuka utepe katika nafasi ya kwanza.

Na sasa kitu cha mwisho ambacho Real Madrid inahitaji baada ya kichapo cha jana ni kupata mechi nyingine ngumu. Lakini kwa bahati mbaya, hivyo ndio kutakuwa siku ya Jumatano watakapocheza nyumbani kwa miamba Sevilla. Real watakuwa bila ya huduma za Sergio Ramos aliyerambishwa kadi nyekundu jana, na pia Angel Di Maria ambaye amekusanya kadi nyingi za njano. Siku hiyo hiyo, viongozi Atletico Madrid watacheza nyumbani dhidi ya Granada. Mapema Jumatano, Barcelona watawaalika Celta Vigo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu