1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AU yairejesha Mali katika umoja wake

Admin.WagnerD25 Oktoba 2012

Umoja wa Afrika umeirudisha tena Mali kuwa mwanachama wa Umoja huo baada ya kuisimamisha kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi mwaka huu. Pamoja na hayo Umoja huo umeunga mkono mipango ya kukomboa eneo la kaskazini.

https://p.dw.com/p/16W9X
African Union Chief Nkosazana Dlamini-Zuma (front L) and Mali's President Dioncounda Traore attend a high level international meeting in Bamako, October 19, 2012. Regional leaders joined international organisations in Bamako on Friday trying to narrow their differences over whether al Qaeda-linked Islamists in the north of Mali should be dislodged via military intervention or a more gradual political approach. REUTERS/Adama Diarra (MALI - Tags: POLITICS)
Ujumbe wa uliyotembelea MaliPicha: Reuters

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayehusika na amani na usalama Ramtane Lamamra aliwaambia waandishi habari kwamba Umoja hup umeamua kuondoa hatua yake ya kuisimamisha Mali kama mwanachama iliochukuliwa miezi saba iliopita mara tu baada ya jeshi kutwaa madaraka  kwa njia ya mapinduzi na kuiangusha serikali ilochaguliwa kidemokrasi.

Mapinduzi hayo yaliwafungulia njia waasi wa Kituareg wakiungwa mkono na Waislamu wa siasa kali kutwaa  mamlaka ya eneo la kaskazini, ukiwemo mji wa kihistoria wa Timbuktu .

Hofu yaongezeka zaidi

Hivi sasa  kukiwa na hofu kwamba eneo hilo lililosawa na Ufaransa linaweza kuwa mahala pa kujihifadhi  Waislamu wenye mafungamano na Al Qaeda, majirani wa Mali na nchi za magharibi wameanzia kuchukua hatua ya kijeshi kulikomboa eneo hilo na kuondowa kitisho hicho.

Akizungumzia suala hilo, Rais wa halmashauri kuu ya Umoja  wa Afrika bibi Nkosozana Dlamini Zuma alisema "Jumatano iliopita Umoja wa Afrika pia uliidhinisha mpango huo na kusisitiza juu ya kurejeshwa kwa mamlaka ya eneo hilo kwa  serikali ya Mali".

African Union Chief Nkosazana Dlamini-Zuma (front L) and Mali's President Dioncounda Traore attend a high level international meeting in Bamako, October 19, 2012. Regional leaders joined international organisations in Bamako on Friday trying to narrow their differences over whether al Qaeda-linked Islamists in the north of Mali should be dislodged via military intervention or a more gradual political approach. REUTERS/Adama Diarra (MALI - Tags: POLITICS)
Nkosazana Dlamini-Zuma na rais wa Mali Dioncounda TraorePicha: Reuters

Wiki iliopita  maafisa wa Umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika, Mali yenyewe na  Jumuiya ya uchumi ya Afrika magharibi ECOWAS walikutana katika mji mkuu wa Mali Bamako kuandaa mkakati wa kuwashinda waasi huko kaskazini.

Jumuiya ya ECOWAS imeandaa kikosi cha wanajeshi wapatao 3,000, kwa shughuli hiyo.

Nchi kadhaa za magharibi ikiwemo Ufaransa zimejitolea kukisaidia kikosi hicho kwa mikakati ya kijeshi na fedha huku Ujeruamani ikisema itakuwa tayari kutoa mafunzo  kwa wanajeshi hao.

Msalaba mwekundu latoa onyo

Wakati huo huo , Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu likionya juu ya janga linalowakumba wakaazi wa Kaskazini mwa Mali, ambako kuna wasiwasi wa kuzuka tatizo la chakula.

Rais wa  Shirika hilo Peter Maurer ambaye amerejea kutoka ziara ya siku tatu katika eneo hilo, amesema mgogoro wa  kaskazini mwa Mali unaweza kusababisha  hali mbaya ya binaadamu katika eneo hilo zima la Sahel. Akaongeza kwamba wakaazi wengi wa kaskazini mwa nchi hiyo wanakimbilia kusini au katika nchi jirani za Niger, Mauritania, Burkina Faso na Algeria na wanahitaji msaada wa dharura.

Hali imezidi kuwa ya kutisha kutokana na taarifa kwamba mamia ya wapiganaji wa Kiislamu kutoka Sudan na Sahara magharibi wamewasili kaskazini mwa Mali mwishoni mwa Juma lililopita, kuyaunga mkono makundi ya Kiislamu, wakijiandaa kukabiliana na uvamizi wa kijeshi.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman,afp
Mhariri: Mohammed Khelef