1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba mtakatifu azungumzia madhila chini ya utawala wa kinazi

20 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/Dkzz

NEW YORK

Kwa mara ya kwanza Kiongozi wa kanisa katoliki duniani baba mtakatifu Benedekti wa 16 amezungumzia mateso aliyoyapitia wakati wa ujana wake chini ya utawala wa kinazi nchini Ujerumani. Akihutubia maelfu ya vijana wa kikatoliki mjini New York aliwatolea mwito kuwa na imani ya kidini kutokana na kuwa na uhuru kufanya hivyo kinyume na yeye alipokuwa kijana alikosa uhuru wa kuwa na imani ya kidini kwa kuwa maisha yake ya ujana yaligubikwa na utawala wenye maovu.

Kiongozi huyo wa kikatoliki leo ataongoza maombi kwenye eneo la World Trade Centre kulikotokea mashambulio ya kigaidi ya mwaka 2001 kama sehemu mojawapo ya maombi ya kuitakia amani Marekani.Baadae leo hii ataongoza misa ya waumini kutoka sehemumbali mbali za Marekani katika uwanja wa Yankee kabla ya kukamilisha ziara yake hii ya kihistoria ya siku sita nchini humo.