1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bado NEC yataka wapigakura wasikae mita 100

Hawa Bihoga14 Oktoba 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imerejelea onyo lake kwa vyama vya siasa kuacha kuwahamasisha wapigakura kukaa karibu na vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura zao.

https://p.dw.com/p/1Gn8R
Wafuasi wa wagombea mbalimbali wa nafasi za uongozi nchini Tanzania.
Wafuasi wa wagombea mbalimbali wa nafasi za uongozi nchini Tanzania.Picha: Getty Images/AFP/D. Hayduk

NEC inasema madai ya kukaa kituoni kwa madai ya kulinda kura kunakwenda kinyume na sheria kanuni na maadili ya uchaguzi pamoja na kuhatarisha usalama.

Tume hiyo ilikuwa inazungumza katika mkutano wake wa mwisho na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam uliolenga kuwakutanisha viongozi wa vyama vya siasa kuelezea maandalizi ya uchaguzi na namna NEC itakavyotumia utaratibu wa kutangaza matokeo ya udiwani, ubunge pamoja na urais.

Sikiliza ripoti ya Hawa Bihoga hapo chini.