1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bado siku nne uchaguzi Ujerumani

19 Septemba 2013

Zaidi ya robo ya wapiga kura wa Ujerumani wamepiga kura zao kabla ya uchaguzi utakaofanyika Jumapili ijayo,kwa mujibu wa maafisa,ikiwa leo(19.09.2013)ni mwisho wa kura zinazopigwa na kutumwa kwa njia ya posta.

https://p.dw.com/p/19kkr
02.09.2013 DW BuWa13 IGD KISUAHELI
Alama ya uchaguzi nchini Ujerumani kwa lugha ya Kiswahili

Na pia chama kipya cha AfD kinachopinga muungano wa Ulaya kinaelekea kupata uwezekano wa kuingia katika bunge la Ujerumani kwa mara ya kwanza. Taarifa zaidi na Sekione Kitojo.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la DPA katika zaidi ya miji 20 mikubwa ya Ujerumani , umegundua kuwa maafisa wa uchaguzi wanaripoti ongezeko kubwa la kura zilizopigwa kwa njia ya posta, ikilinganishwa na mwaka 2009, wakati asilimia 21.4 ya wale waliopiga kura zao walipata karatasi za kura kabla na kuzirejesha kwa njia ya posta.

The top-candidate of the left-wing Die Linke party Gregor Gysi speaks during an election campaign rally in Leipzig, August 28, 2013. German voters will take to the polls in a general election on September 22. REUTERS/Thomas Peter (GERMANY - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Mgombea wa chama kidogo cha Die LinkePicha: Reuters

Kura yoyote ambayo haitarejeshwa katika ofisi ya tume ya uchaguzi ifikapo saa 12 jioni kwa saa za Ulaya ya kati siku ya Jumapili haitahesabiwa. Maafisa wa shirikisho wanashauri kwamba kura hizo zitumwe kwa njia ya posta leo Alhamis(19.09.2013) ili kuhakikisha kuwa zinafika katika wakati muafaka.

Kura kupitia posta

Ujerumani inaruhusu upigaji wa kura kupitia posta kutokea nyumbani ama wakati mtu yuko safarini , kama njia mbadala ya kujipanga mstari katika vituo vya kupigia kura siku ya Jumapili. Kiasi ya wapigakura milioni 9.4 walitumia njia hiyo ya posta mwaka 2009. Ujerumani ina wapiga kura milioni 61.8 waliojiandikisha kupiga kura mwaka huu.

Wakati huo huo chama kipya kinachopinga muungano wa Ulaya kiko ukingoni mwa kuingia katika bunge la Ujerumani kwa mara ya kwanza , umeonesha uchunguzi wa maoni ya wapiga kura , na kuweka kiwingu kwa juhudi za kansela Angela Merkel kuendeleza muungano wake wa siasa za wastani za mrengo wa kulia na kukwaza sera zake za eneo la sarafu ya euro.

Merkel ana hakika

Merkel bado ana hakika ya kupata kipindi cha tatu cha uongozi katika uchaguzi wa hapo Jumapili. Lakini chama chagua mbadala kwa Ujerumani AfD, ambacho kinanyanyuliwa kutokana na wimbi upinzani kuhusu msaada wa uokozi kwa mataifa yenye madeni ya upande wa kusini mwa Ulaya , kinaweza kuligawa zaidi bunge la Ujerumani , na kumlazimisha Merkel kuunda muungano wa serikali na mahasimu wake wa Social Democratic , SPD , katika kile kinachoelezwa kuwa muungano mkuu wa siasa za mrengo wa kulia na kushoto.

ARCHIV - ILLUSTRATION - SPD- und CDU-Parteifähnchen vor dem Reichstag in Berlin (Archivfoto vom 20.09.2005, Illustration zum Thema Große Koalition). Foto: Gero Breloer dpa (dpa Serie "Bundestagswahl historisch"; zu dpa "2005: Schröder am Ende - Merkel führt große Koalition" vom 05.09.2013) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Bango la uchaguzi wa chama cha SPD na CDUPicha: picture-alliance/dpa

Kukubalika kwa chama hicho , ambacho kinapendelea kuyaondoa mataifa dhaifu kutoka uanachama wa sarafu ya euro , utaleta hali ya hofu miongoni mwa mataifa ya Ulaya na hali hiyo inaweza kuzusha wasi wasi pia katika masoko ya fedha, licha ya kuwa sauti yake katika bunge bado itakuwa ndogo.

Lakini wanachama wa chama cha kansela Angela Merkel wamebadilisha mbinu sasa siku nne kabla ya uchaguzi na wanakishambulia chama hicho.

Chama cha kansela Angela Merkel cha Christian Democratic ambacho kilikidharau chama hicho kidogo cha AfD katika kampeni hadi sasa, kimemuweka mtu wao maarufu kabisa , waziri wa fedha Wolfgang Schauble kukishughulikia chama hicho kipya.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (M, CDU) spricht am 18.09.2013 zu Beginn der Sitzung des Bundeskabinetts im Bundeskanzleramt in Berlin mit Bundesministerin für Arbeit und Soziales, Ursula von der Leyen (vl, CDU), Bundesaußenminister Guido Westerwelle (FDP), Bundeswirtschaftsminister Philipp Rösler (FDP, verdeckt), Kanzleramtsminister Ronald Pofalla (CDU), Staatsminister Eckart von Klaeden und Kultur-Staatsminister Bernd Neumann. Es ist die letzte Kabinettssitzung vor der Bundestagswahl am 22. September 2013. Foto: Kay Nietfeld/dpa
Kikao cha baraza la sasa la mawaziri pamoja na kansela Merkel mjini BerlinPicha: picture-alliance/dpa

"Watu hawa wanadai kuwa tutakuwa katika hali bora zaidi ikiwa tutaachana na sarafu ya euro", waziri huyo mwenye umri wa miaka 71 ameliambia gazeti la Die Welt. Madai hayo si ya kweli kabisa, hayana ukweli na ni hatari sana kwa ustawi wetu. amemaliza Schauble.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae

Mhariri: Josephat Charo