1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Al-Qaeda yadai kuhusika na mauaji ya Abu Reesha

15 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPf

Tawi la mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda nchini Irak limesema kuwa lilifanya shambulizi lililomuuwa kiongozi mashuhuri wa Kisunni,Abdul Sattar Abu Reesha katika Wilaya ya Al-Anbar.Abu Reesha alikuwa akiongoza kundi linaloshirikiana na majeshi ya Marekani kupambana na magaidi wa Al-Qaeda katika wilaya ya Anbar.

Juma lililopita,Rais wa Marekani,George W.Bush alikutana na Abu Reesha,alipofanya ziara yake ya ghafula nchini Irak.