1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Jengo la bunge lalipuliwa.

13 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAN

Mtu aliyejitoa muhanga amejilipua katika jengo la bunge la Iraq ambalo liko katika eneo ambalo linalindwa sana na linalojulikana kama zoni ya kijani mjini Baghdad, na kuuwa kiasi watu wanane na wengine 20 wamejeruhiwa.

Mlipuko huo ulitokea katika mkahawa uliokuwa na watu wengi.

Kiasi watu watatu ambao wameuwawa ni wabunge. Rais wa Marekani George W. Bush amesema kuwa tukio hilo linaonyesha jinsi wapiganaji nchini Iraq walivyo.

Hapo mapema , kiasi watu kumi waliuwawa na wengine kadha kujeruhiwa wakati gari lililokuwa na milipuko lilipoharibu daraja muhimu katika mto Tigris. Magari kadha yalitumbukia katika mto huo wakati daraja hilo lilipovunjika.