1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Mabomu yaua watu 14 nchini Iraq.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmB

Mabomu matatu yamelipuka wakati mmoja karibu na kituo cha kuuzia mafuta katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, na kuuwa watu 14.

Shambulio hilo lilitokea katika eneo linalokaliwa zaidi na Washia la Bayaa.

Katika tukio jingine , wafanyakazi wa kidini wa Kishia wameuwawa katika shambulio la ghafla katika basi.

Jeshi la Marekani limesema kuwa wapiganaji wameshambulia magari ya doria ya jeshi hilo mjini Baghdad, na kumuua mwanajeshi mmoja na kuwajeruhi wengine watano.

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki amekanusha maelezo yaliyotolewa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan. Siku ya Jumapili, Annan ameieleza hali nchini Iraq kuwa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kusema wakaazi wana wasi wasi zaidi wa kutoka katika majumba yao kuliko wakati wa dikteta Saddam Hussein.

Maelezo hayo pia yamekosolewa na wataalamu wa masuala ya sera za kigeni katika serikali ya mseto ya Ujerumani, Eckart von Klaeden na Ulrich Klose.