1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Marekani yaishutumu Iran kwa mashambulio dhidi ya wanajeshi

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmR

Jeshi la Marekani limeishutumu Iran kwa kuhusika na mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Marekani walio nchini Irak.

Brigedia jenerali Kevin J Bergner wa jeshi la Marekani amesema Iran inataka kuunda upinzani kama ule wa kundi la Hezbolah la Lebanon ili kupambana na wanajeshi wa Marekani na wa Irak.

Msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni wa Iran ameyaeleza madai hayo kuwa ya kushangaza.

Sambamba na hayo wanajeshi wa Marekani nchini Irak wamewaua wanamgambo wawili wa kiislamu na kuwakamata wengine wanane kwenye operesheni iliyofanywa mjini Baghdad hapo jana. Wanajeshi hao pia waligundua maficho ya mabomu.

Msemaji wa jeshi la Marekani nchini Irak, luteni kanali Christopher Garver, amesema wanataka kuuangamiza mtandao wa mashambulio ya mabomu yanayofanywa na watu kujitoa mhanga maisha.