1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulizi yameua hadi watu 12 nchini Irak

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXd

Watu wasiopungua 12 wameuawa na wengine 31 wamejeruhiwa katika shambulizi la makombora lililofanywa mashariki ya mji mkuu Baghdad leo Jumapili.Kwa mujibu wa afisa mmoja katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Irak,shambulizi hilo lilifanywa wakati wa mapambano makali kati ya wanajeshi wa Kimarekani na wanamgambo katika mtaa wa Obaidi,eneo wanakoishi Washia wengi.