1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Mkutano wa usalama wa Iraq wafunguliwa

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKW

Mkutano wa ngazi ya juu ya usalama wa Iraq unaohudhuriwa na nchi jirani za Iraq na nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umefunguliwa mjini Baghdad leo hii.

Mkutano huo una lengo la kuzihusisha zaidi nchi jirani na Iraq kuleta utulivu nchini humo kwa kukomesha umwagaji damu wa kimadhebu kabla ya kuenea katika eneo zima la Mashariki ya Kati.

Nadhari imekuwa juu ya tetesi iwapo kutakuwapo na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Marekani, Iran na Syria pembezoni mwa mkutano huo.Mazungumzo hayo yanaonyesha kubadilika kwa sera ya Marekani kutokana na utawala wa Rais George W. Bush kugoma hadi sasa kuwasiliana moja kwa moja na Iran na Syria ambazo inazishutumu kwa kuunga mkono uasi nchini Iraq.