1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Raia wanne wauwawa kwenye operesheni ya jeshi la Marekani

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZN

Maafisa nchini Irak wanasema raia wanne, akiwemo msichana wa miaka mitatu, wameuwawa leo wakati wa operesheni ya pamoja iliyofanywa na jeshi la Marekani na vikosi vya Irak katika wilaya ya Sadr mjini Baghdad.

Jeshi la Marekani kwa upande wake limesema wanamgambo wanne wameuwawa wakati wa ufyatulianaji wa risasi na halina habari zozote kuhusiana na vifo hivyo vya raia.

Raia hao wameuwawa wakati wanajeshi wa Marekani na wa Irak wakisaidiwa na helikopta walipofanya msako wa nyumba kwa nyumba kuanzia saa tisa usiku wa kuamkia leo mashariki mwa Baghdad.

Makamanda wa Marekani wanahofu wanamgambo huenda wakaongeza mashambulio yao dhidi ya wanajeshi wa Marekani au kuwashambulia raia kujaribu kubadili mkondo wa mazungumzo mjini Washington kuhusu vita nchini Irak.