1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Ripoti za kutatanisha kuhusu Abu Ayyub al-Masri

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRa

Maafisa wa majeshi wa Kimarekani nchini Irak wamekanusha ripoti zilizodai kuwa kiongozi wa tawi la Al-Qaeda nchini Irak,Abu Ayyub al-Masri,amejeruhiwa au ameuawa katika mapigano na vikosi vya Kiiraki kaskazini mwa mji mkuu Baghdad.Hapo awali,kaskazini mwa mji mkuu Baghdad msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Irak alisema kuwa al-Masri amejeruhiwa.Al-Masri alie mzaliwa wa Misri,alishika uongozi wa tawi hilo la Al-Qaeda,baada ya mwanamgambo wa Kijordan Abu-Musab al-Zarqawi kuuawa Juni mwaka jana,katika shambulio la angani la Marekani.