1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Saddam Hussein azikwa

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCeZ

Kiongozi wa zamani wa Irak, Saddam Hussein, amezikwa katika kijiji chake cha Awja karibu na mji wa Tikrit kaskazini mwa Irak. Mazishi yamefanyika kabla alfajiri chini ya masaa 24 tangu aliponyongwa.

Wana wawili wa kiume wa Saddam, Uday na Qusay, waliouwawa na wanajeshi wa Marekani mnamo mwaka wa 2003, walizikwa katika uwanja wa familia yao katika kijiji hicho cha Awja.

Saddam mwenye umri 69 alihukumiwa kunyongwa na mahakama ya Irak mwezi uliopita kwa kuhusika katika mauaji ya wairaki takriban 148 kwenye kijiji cha washia cha Dujail mnamo mwaka wa 1982.

Wakati haya yakiarifiwa majeshi ya Irak na ya Marekani yamewekwa katika hali ya tahadhari kufuatia kunyongwa kwa Saddam Hussein. Mashambulio ya mabomu ya kutegwa ndani ya magari yamewauwa watu wasiopungua 70 katika maeneo yanayokaliwa na washia nchini Irak.

Wairaki wengine wengi wamejeruhiwa katika milipuko ya mabomu, mlipuko mbaya zaidi ukitokea katika mji wa Washia wa Kufa, yapata kilomita 160 kusini mwa mji mkuu Baghdad.